Na
Paschazia Charles
Uzinduzi wa mashindano ya Dindai Cup umefanyika leo June1, 2026 katika uwanja wa Pepsi uliopo kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Akizungumza katika hafla hiyo Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa mashindano hayo Bi. Lilian Kashega ambaye ni Mkaguzi wa POLISI kata ya Chamaguha amewataka Vijana kuacha kujihusisha na tabia zisizo na faida ikiwemo ulevi, uvutaji wa madawaya kulevya.
Pia ameiasa jamii kuachana na vitendo vya ukatili kwa wengine wakiwemo watoto, Wananwake na jamii mzima.
Kwa upande wao Viongozi wa Chama Cha mpira Wilaya ya Shinyanga SHIDIFA wameishukuru Mfadhili wa mashindano hayo na kwamba ameeandaa mashino hayo lengo kubwa ni kuinua vipaji vya Vijana wadogo katika Manispaa ya Shinyanga.
Timu shiriki katika mashindano hayo ya Dindai Cup ni Chamaguha Fc, C-Coy Sc, Busulwa Sports Academy, Katunda Fc, Chipukizi Fc, Iwelyangula Fc, Home Boys Fc, Kabondo Fc katika msimu huu wa mashindano ya DINDAI CUP 2026.
Katika mechi ya ufunguzi siku ya leo kati ya Chamaguha vs Kabondo Fc kutoka Galaba Kolandoto imemalizika kwa suruhu na mechi ya marudianao itafanyika siku ya ijumaa June 5,2026 katika uwanja wa Pepsi Kata ya Chamagua
Siku ya kesho mashindano yataendelea kati ya Iwelwangulya vs Home Boys katika uwanja wa Pepsi Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.













